Habari za Punde

Rais Kikwete Atua Zanzibar Kufariji Waliopatwa na Maafa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali leo July 19, 2012.



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, wakipata maelezo kutoka kwa daktari wa jeshi la Polisi anaeshughulikia vinasaba (DNA), Dk. Ahmed Makata, alipofika katika eneo la kuhifadhia maiti wa ajali ya kuzama meli ya MV.Skagit, kwenye viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012

Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi leo July 19, 2012. 

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.