Habari za Punde

DK Bilal afariji Wafiwa na Wahanga wa ajali ya meli


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, leo Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.